Korosho
ni zao la biashara hapa Tanzania linalostawi vizuri katika ukanda wa pwani;
mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani. Korosho ina matumizi mengi ikiwa ni pamoja na
utengenezaji wa mafuta ya kula, Keki na hutumika pia kama nuts kwa binadamu.
Hata hivyo
mbali na kuwepo kwa matumizi hayo kuna fursa ambayo bado mbichi kutokana na bibo
la korosho ambalo huweza kutengeneza
wine (mvinyo), Juice, Jams na local beer (pombe za kienyeji)
Fursa hii
ya usindikaji wa mabibo ya korosho katika kutengeneza mazao tajwa hapo juu, inahitaji uwekazaji
katika techolojia ili kuweza kusindika bibo hizo na kupata rasimali watu wenye
uwezo katika kufanikisha hilo.
Ni
wakati mzuri kujikita katika fursa hii ili mabibo yanayopotea kuweza kugeuzwa
katika bidhaa ambazo zitatuletea kipato; changamkia Fursa hiyo hapa Naliendele
Mtwara na maeneo yanayozalisha Korosho nchini.
thanks very much for your advice hoping that we can jump from poor to rich via your knowledge stay blessed.
ReplyDelete@ngumbanehemiah