Skip to main content

ONGEZA THAMANI KWA MATUMIZI MBADALA




Ubunifu katika kutafuta na kufanya matumizi mbadala ya vitu mbalimbali ni njia nzuri yenye kuongeza thamani ya vile vitu vinavyoonekana havifai tena kutumiwa katika matumizi yake ya kawaida. Katika kuongeza thamani wakati mwingine imekuwa ni changamoto hasa katika kupata namna ya kutengeneza matumizi hayo mbadala, mjasiriamali yeye hutafsiri na kuchukulia hali hiyo kama fursa kwake, hii ndiyo kazi yake kubwa, ubunifu na kugundua vitu vipya.
Leo tuangalie namna ambavyo Magunia ambayo wakati mwingine hujulikana kwa majina ya viroba au mifuko, yanavyo tengenezwa kuwa Zulia au Capeti au Mapambo ya Ukutani
Kwa kawaida Magunia, katika maeneo mengi hutumika katika kuhifadhi mazao mfano nafaka, bidhaa za viwandani na wakati mwingine pia hutumia kuhifadhia uchafu yabisi.
Nilifanikiwa kumtembelea mjasiriamali mmoja yeye kazi yake ni kutengeza mazulia au carpet (capeti) au Mapambo ya ukutani alisema hivi “Kwa kutumia magunia yaliyo isha matumizi yake ya kawaida au lisilo na matumizi ya kuhifadhia ama maamuzi ya mhitaji mwenyewe, uzi wenye rangi mbalimbali ama kulingana na mhusika anavyo taka yeye (rangi moja) natengeneza(nafuma) mazulia, capeti ya kukanyagia na mapambo ya ukutani kufuatia uhitaji wa mhusika , naweka picha ya kitu anacho hitaji mtu mwenyewe mfano samaki, mtungi, nembo ya kitu fulani au chama nk na naweka pia urembo mwingine pembeni ili lipendeze zaidi.” Mama Salim
Akazungumzia soko lake lilivyo nakusema liko vizuri mpaka sasa kila moja huuzwa sh. 25,000/= Mama Salim.
Umeona hapo, badala ya kulitupa gunia kwamba halifai kwa matumizi yake unaliongezea thamani yake kwa matumizi mbadala kama ambavyo Mjasiriamali (Mama Salim) huyu anavyo fanya.
Je, unahitaji kujua kwa undani zaidi (Kujifunza) au kutengenezewa? Ni wasaa mzuri kwako kujipatia la kwako, au kujifunza juu ya fursa hii ili kuongeza thamani ya magunia na kutoa huduma hiyo.
Kwa mawasiliano zaidi tupigie/tuma ujumbe mfupi kupitia:
Mama salim
0719907076
Heneriko S. Muhagaze
0654597780

Comments

Popular posts from this blog

USINDIKAJI WA MABIBO YA KOROSHO: Naliendele-Mtwara

Korosho ni zao la biashara hapa Tanzania linalostawi vizuri katika ukanda wa pwani; mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani. Korosho ina matumizi mengi ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa mafuta ya kula, Keki na hutumika pia kama nuts kwa binadamu. Hata hivyo mbali na kuwepo kwa matumizi hayo kuna fursa ambayo bado mbichi kutokana na bibo la korosho ambalo huweza kutengeneza wine (mvinyo), Juice, Jams na local beer (pombe za kienyeji) Fursa hii ya usindikaji wa mabibo ya korosho katika kutengeneza mazao tajwa hapo juu, inahitaji uwekazaji katika techolojia ili kuweza kusindika bibo hizo na kupata rasimali watu wenye uwezo katika kufanikisha hilo. Ni wakati mzuri kujikita katika fursa hii ili mabibo yanayopotea kuweza kugeuzwa katika bidhaa ambazo zitatuletea kipato; changamkia Fursa hiyo hapa Naliendele Mtwara na maeneo yanayozalisha Korosho nchini.

THE ASPECTS OF MIND:THE MIND OF KASHENGO

THE MIND OF KASHENGO, Continues…… In their minds and hearts, it was the joyful history for their clan, knowing that, their son (Kashengo) would bring an impact on their clan and society as an educated person. Kashengo marked the goo beginning to his society with the high respect, of which everyone would have to tell in his village. He turned the past history into new history; this became the point of interest in people’s minds in that village. Mrs.Mkumbo insisted Kashengo by telling, “my son, it is not enough you have to prepare good environments for your future life, passing the exam is not enough but shaping your mind to master your future life counts”. Kashengo could then continue by feeling great joy having passed the exam and he could receive more gifts from different people. One day he decided to visit his uncle who was living in the same village. When at uncle’s place, Kashengo got information that he had been selected to join at Ngogwa secondary school which

FURSA 5 KUBWA KUFUATIA TAMKO LA SERIKALI WANAFUNZI WOTE KUSOMA SAYANSI.

Mnamo tarehe 7 August 2016, Serikali ilitoa mwongozo mpya wa Elimu kupitia waziri wa Elimu, Sayansi, Technolojia na Mafunzo ya ufundi Prof. Joyce Ndalichako kuwa masomo ya sayansi ni lazima yasomwe na wanafunzi wote. Kufuatia mwongozo huo mbali na kwamba changamoto zipo, fursa kadhaa zimejitokeza ili kulifanikisha tamko hilo ipasavyo, hivyo ni wasaa mzuri kwako kulifuatilia kwa ukaribu mkubwa huenda fursa hizo zikawa zinakuhusu moja kwa moja, tazama hapa chini:   Ajira kwa walimu wa Sayansi ; Kufutia tamko hilo wanahitajika Walimu wengi wa masomo ya Sayansi ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. 2.    Hamasa na motisha kwa wanafunzi ; Kujikita ipasavyo kwenye masomo hayo kwa vitendo tofauti na ilivyo kuwa mwanzoni sababu iliyopelekea wengi kuyaona masomo magumu na suluhu kwa walio wengi ilikuwa kuyakimbia na kujikita kwenye masomo ya sanaa. 3.    Fursa kubwa kwa wauzaji wa kemikali , wenye bustani zenye mimea ya kujifunzia, mabwawa ya s