Skip to main content

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUAMUA KIPI UFANYE MIONGONI MWA FURSA NYINGI.



Katika maisha ya kila siku, mazingira na matukio yanayojitokeza katika jamii ni mwanya wa kufanya jambo kubwa sana, ni fursa kwako. Ili Kuishi kwa malengo na hatimae kuishi ndoto ni lazima kujifunza kutafsiri kila hali na kugeuza matatitizo yaliyopo kuwa fursa zenye tija kwako na jamii inayokuzunguka. Wakati wengine wakihangaika kutafuta biashara inayolipa wewe unajitaabisha kutafuta tatizo ili ulifumbue! watu huhitaji majawabu ya kile kinacho wasumbua kila siku, Hutawatafuta watumiaji bali utatafutwa kwa kile ulicho kifanya.
Hii ni muhimu kwa sababu ukiwa huna sehemu uliyojishikiza, utapelekwa na upepo kokote uendako, maana yake lazima uamue kuwa na shughuli unayoifanya hata kama unaiona ndogo,  mimi nakuambia hiyo ni kubwa ukiifanya kwa hekima, kwa kujituma na ukiithamini kwa namna zote itafungua milango ya shughuli zingine nzuri zaidi.
Mambo ya kuzingitia katika kuchagua kipi ufanye, Ukizingatia hali halisi ya uhitaji wa mazingira uliyopo.
1.   Anza kuchunguza soko kabla ya kitu chochote kile, Hili litakuwezesha kujua ni kipi ukifanya kitakulipa, Na pia huweza hata kukufahamisha kuwa hata wazo ulilokuwa nalo (unaliamini) sasa soko lake si zuri hivyo unahirisha kuzalisha/ kufanya shughuli hiyo kwasababu inaweza kuingizia hasara kama utalazimisha kufanya. Huu ndio uzuri wa kuanzia kwenye soko badala ya kuzalisha kwanza halafu unatafuta soko. Kwa mfano ukiamua kufuga kuku chunguza kwa makini soko likoje sasa na mwelekeo wake siku za usoni upoje kabla  ya kuamua kwamba sasa nafuga kuku wa kienyeji au chotara au wa mayai/nyama.
2.  Ukitoka sokoni, amua nini sasa ufanye kama biashara yako au shughuli yenye tija. Mategemeo yatakuwa sasa umeweza kujua nini kinahitajika sokoni na uhitaji huo ni wa mda gani mpaka uishe. Chagua shughuli itakayo kuingizia faida zaidi, weka ubunifu ili iwe bora kuvutia soko (watumiaji)
3.  Soko linahitaji kiasi gani, hapa unahitsaji kujua ni kiasi gani uweze kuzalisha au shughuli yako iwe kwa kiasi gani ili kukidhi mahitaji yaliyopo kwa sasa na siku za usoni
4.  Weka mpango mkakati namna utakavyo fanikisha shughuli hiyo mfano ukiamua kufuga kuku wa kienyeji inabidii ujue mahitaji muhimu ya kuku wa kienyeji na taratibu zake ili usingie hasara; namna ya kuwalisha, sehemu bora ya kuwafugia, kuwakinga na magonjwa kwa wakati, usimamizi mzuri nk
5.  Fanya shughuli hiyo kwa kumaanisha na kujituma (Fanya kwa biddi) Shughuli yoyote iliyo halali hulipa kulingana na mrejesho wake wa faida ulivyo (ukubwa kwa shughuli). Sehemu kubwa ambayo wengi tunaharibu ni kwamba tunafanya kama tunamfanyia mtu mwingine hata kama kitu ni chetu wenyewe. Ebu wewe leo ifanye shughuli yako kwa bidii na kumaanisha  katika usimamizi na uwezeshaji itakulipa sana hutaamini, maana yake uwezo wa kusimamia ulionao ni kitu muhimu kuzingatia katika shughuli uliyoichagua kama unataka kuifanikisha vizuri.
6.   Ifanye ijulikane na maeneo uliyolenga kama soko lako hii itasadia kuweza kuvuta makini ya wahitaji wa bidhaa unazo zalisha kama hukuingia mkataba na soko husika wakati wa kuzalisha. Pia kupitia watu wa karibu yako katika maeneo mbalimbali sambaza ujumbe wa bidhaa hizo ili kuwaanda kisaikolojia juu ya ujio wako.
7.   Anza kusambaza mazao ya shughuli uliyo kuwa ukifanya kaika masoko husika. unaweza kusambaza kwa order au mwenyewe kuwa unampelekea mtumiaji moja kwa moja (unasambaza). Inategemea shughuli yako inalinganaje na inahitaji soko kiasi gani.
UHITAJI WETU NI SULUHU YA MATATIZO YANAYOTUKUMBA, KUWA SEHEMU YA WATATUZI KWA MAFANIKIO YAKO NA JAMMI NZIMA.



Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

USINDIKAJI WA MABIBO YA KOROSHO: Naliendele-Mtwara

Korosho ni zao la biashara hapa Tanzania linalostawi vizuri katika ukanda wa pwani; mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani. Korosho ina matumizi mengi ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa mafuta ya kula, Keki na hutumika pia kama nuts kwa binadamu. Hata hivyo mbali na kuwepo kwa matumizi hayo kuna fursa ambayo bado mbichi kutokana na bibo la korosho ambalo huweza kutengeneza wine (mvinyo), Juice, Jams na local beer (pombe za kienyeji) Fursa hii ya usindikaji wa mabibo ya korosho katika kutengeneza mazao tajwa hapo juu, inahitaji uwekazaji katika techolojia ili kuweza kusindika bibo hizo na kupata rasimali watu wenye uwezo katika kufanikisha hilo. Ni wakati mzuri kujikita katika fursa hii ili mabibo yanayopotea kuweza kugeuzwa katika bidhaa ambazo zitatuletea kipato; changamkia Fursa hiyo hapa Naliendele Mtwara na maeneo yanayozalisha Korosho nchini.

THE ASPECTS OF MIND:THE MIND OF KASHENGO

THE MIND OF KASHENGO, Continues…… In their minds and hearts, it was the joyful history for their clan, knowing that, their son (Kashengo) would bring an impact on their clan and society as an educated person. Kashengo marked the goo beginning to his society with the high respect, of which everyone would have to tell in his village. He turned the past history into new history; this became the point of interest in people’s minds in that village. Mrs.Mkumbo insisted Kashengo by telling, “my son, it is not enough you have to prepare good environments for your future life, passing the exam is not enough but shaping your mind to master your future life counts”. Kashengo could then continue by feeling great joy having passed the exam and he could receive more gifts from different people. One day he decided to visit his uncle who was living in the same village. When at uncle’s place, Kashengo got information that he had been selected to join at Ngogwa secondary school which

FURSA 5 KUBWA KUFUATIA TAMKO LA SERIKALI WANAFUNZI WOTE KUSOMA SAYANSI.

Mnamo tarehe 7 August 2016, Serikali ilitoa mwongozo mpya wa Elimu kupitia waziri wa Elimu, Sayansi, Technolojia na Mafunzo ya ufundi Prof. Joyce Ndalichako kuwa masomo ya sayansi ni lazima yasomwe na wanafunzi wote. Kufuatia mwongozo huo mbali na kwamba changamoto zipo, fursa kadhaa zimejitokeza ili kulifanikisha tamko hilo ipasavyo, hivyo ni wasaa mzuri kwako kulifuatilia kwa ukaribu mkubwa huenda fursa hizo zikawa zinakuhusu moja kwa moja, tazama hapa chini:   Ajira kwa walimu wa Sayansi ; Kufutia tamko hilo wanahitajika Walimu wengi wa masomo ya Sayansi ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. 2.    Hamasa na motisha kwa wanafunzi ; Kujikita ipasavyo kwenye masomo hayo kwa vitendo tofauti na ilivyo kuwa mwanzoni sababu iliyopelekea wengi kuyaona masomo magumu na suluhu kwa walio wengi ilikuwa kuyakimbia na kujikita kwenye masomo ya sanaa. 3.    Fursa kubwa kwa wauzaji wa kemikali , wenye bustani zenye mimea ya kujifunzia, mabwawa ya s