Skip to main content

FURSA 5 KUBWA KUFUATIA TAMKO LA SERIKALI WANAFUNZI WOTE KUSOMA SAYANSI.



Mnamo tarehe 7 August 2016, Serikali ilitoa mwongozo mpya wa Elimu kupitia waziri wa Elimu, Sayansi, Technolojia na Mafunzo ya ufundi Prof. Joyce Ndalichako kuwa masomo ya sayansi ni lazima yasomwe na wanafunzi wote. Kufuatia mwongozo huo mbali na kwamba changamoto zipo, fursa kadhaa zimejitokeza ili kulifanikisha tamko hilo ipasavyo, hivyo ni wasaa mzuri kwako kulifuatilia kwa ukaribu mkubwa huenda fursa hizo zikawa zinakuhusu moja kwa moja, tazama hapa chini:
  1.  Ajira kwa walimu wa Sayansi; Kufutia tamko hilo wanahitajika Walimu wengi wa masomo ya Sayansi ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
2.   Hamasa na motisha kwa wanafunzi; Kujikita ipasavyo kwenye masomo hayo kwa vitendo tofauti na ilivyo kuwa mwanzoni sababu iliyopelekea wengi kuyaona masomo magumu na suluhu kwa walio wengi ilikuwa kuyakimbia na kujikita kwenye masomo ya sanaa.
3.   Fursa kubwa kwa wauzaji wa kemikali, wenye bustani zenye mimea ya kujifunzia, mabwawa ya samaki, na viumbe wengine wa majini kwa matumizi  wakati wa kusoma kwa vitendo
4.   Ujenzi na upanuzi wa maabara za kujifunzia mashuleni, Kwa wauzaji wa vifaa vya ujenzi na Fundi uashi nchini ni nafasi kwao kujizatiti ipasavyo katika fursa hii.
5.   Uhitaji wa Vitabu vya kujifunzia masomo ya Sayansi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, Waandishi wa vitabu vya masomo ya sayansi ni fursa kubwa kwao ili kukidhi uhitaji ulipo mashuleni.

Comments

Popular posts from this blog

USINDIKAJI WA MABIBO YA KOROSHO: Naliendele-Mtwara

Korosho ni zao la biashara hapa Tanzania linalostawi vizuri katika ukanda wa pwani; mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani. Korosho ina matumizi mengi ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa mafuta ya kula, Keki na hutumika pia kama nuts kwa binadamu. Hata hivyo mbali na kuwepo kwa matumizi hayo kuna fursa ambayo bado mbichi kutokana na bibo la korosho ambalo huweza kutengeneza wine (mvinyo), Juice, Jams na local beer (pombe za kienyeji) Fursa hii ya usindikaji wa mabibo ya korosho katika kutengeneza mazao tajwa hapo juu, inahitaji uwekazaji katika techolojia ili kuweza kusindika bibo hizo na kupata rasimali watu wenye uwezo katika kufanikisha hilo. Ni wakati mzuri kujikita katika fursa hii ili mabibo yanayopotea kuweza kugeuzwa katika bidhaa ambazo zitatuletea kipato; changamkia Fursa hiyo hapa Naliendele Mtwara na maeneo yanayozalisha Korosho nchini.

THE ASPECTS OF MIND:THE MIND OF KASHENGO

THE MIND OF KASHENGO, Continues…… In their minds and hearts, it was the joyful history for their clan, knowing that, their son (Kashengo) would bring an impact on their clan and society as an educated person. Kashengo marked the goo beginning to his society with the high respect, of which everyone would have to tell in his village. He turned the past history into new history; this became the point of interest in people’s minds in that village. Mrs.Mkumbo insisted Kashengo by telling, “my son, it is not enough you have to prepare good environments for your future life, passing the exam is not enough but shaping your mind to master your future life counts”. Kashengo could then continue by feeling great joy having passed the exam and he could receive more gifts from different people. One day he decided to visit his uncle who was living in the same village. When at uncle’s place, Kashengo got information that he had been selected to join at Ngogwa secondary school which