Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2016

ONGEZA THAMANI KWA MATUMIZI MBADALA

Ubunifu katika kutafuta na kufanya matumizi mbadala ya vitu mbalimbali ni njia nzuri yenye kuongeza thamani ya vile vitu vinavyoonekana havifai tena kutumiwa katika matumizi yake ya kawaida. Katika kuongeza thamani wakati mwingine imekuwa ni changamoto hasa katika kupata namna ya kutengeneza matumizi hayo mbadala, mjasiriamali yeye hutafsiri na kuchukulia hali hiyo kama fursa kwake, hii ndiyo kazi yake kubwa, ubunifu na kugundua vitu vipya. Leo tuangalie namna ambavyo Magunia ambayo wakati mwingine hujulikana kwa majina ya viroba au mifuko, yanavyo tengenezwa kuwa Zulia au Capeti au Mapambo ya Ukutani Kwa kawaida Magunia, katika maeneo mengi hutumika katika kuhifadhi mazao mfano nafaka, bidhaa za viwandani na wakati mwingine pia hutumia kuhifadhia uchafu yabisi. Nilifanikiwa kumtembelea mjasiriamali mmoja yeye kazi yake ni kutengeza mazulia au carpet (capeti) au Mapambo ya ukutani alisema hivi “ Kwa kutumia magunia yaliyo isha matumizi yake ya kawaida au lisilo na matu

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUAMUA KIPI UFANYE MIONGONI MWA FURSA NYINGI.

Katika maisha ya kila siku, mazingira na matukio yanayojitokeza katika jamii ni mwanya wa kufanya jambo kubwa sana, ni fursa kwako. Ili Kuishi kwa malengo na hatimae kuishi ndoto ni lazima kujifunza kutafsiri kila hali na kugeuza matatitizo yaliyopo kuwa fursa zenye tija kwako na jamii inayokuzunguka. Wakati wengine wakihangaika kutafuta biashara inayolipa wewe unajitaabisha kutafuta tatizo ili ulifumbue! watu huhitaji majawabu ya kile kinacho wasumbua kila siku, Hutawatafuta watumiaji bali utatafutwa kwa kile ulicho kifanya. Hii ni muhimu kwa sababu ukiwa huna sehemu uliyojishikiza, utapelekwa na upepo kokote uendako, maana yake lazima uamue kuwa na shughuli unayoifanya hata kama unaiona ndogo,   mimi nakuambia hiyo ni kubwa ukiifanya kwa hekima, kwa kujituma na ukiithamini kwa namna zote itafungua milango ya shughuli zingine nzuri zaidi. Mambo ya kuzingitia katika kuchagua kipi ufanye, Ukizingatia hali halisi ya uhitaji wa mazingira uliyopo. 1.    Anza kuchunguza soko kabl